TRA YAWAKUMBUKA WALEMAVU MWANZA.
Kwa mara ya kwanza mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)mkoa wa Mwanza imewakumbuka wajasiriamali wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi) na kutoongea (mabubu) kwa kuwaelimisha masuala ya ujasiriamali,kodi na mbinu za biashara.
Akitoa mada ya ujasiriamali na kodi,ofisa mwandamizi wa huduma na elimu ya kodi wa TRA mkoa wa Mwanza Lutufyo Mtafya, alitaja sifa za mjasiriamalikua ni uwezo,ubunifu,kujiamini,kujituma,kuona fursa na kukabili vikwazo.
Akisisitiza Mtafya alisema wafanya biashara wanapokosa vibali ni wazi kwamba hawezi kupata zabuni kubwa,bila kusita kuwatumia watu wenye uzoefu,vipaji na mtaji.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Mwanza, Jones George na mkalimani kutoka Chama cha Wakalimani wa Lugha ya Alama Tanzania, Subira Joseph, aliupongeza uongozi wa TRA mkoani hapa kutokana na hatua hiyo ya kuwakumbuka walemavu hao katika elimu ya ujasiriamali na kodi.
No comments:
Post a Comment
Phone: +255745767927
Email: jeremiahelijah01@gmail.com
facebook page: OMBLOX